Tuesday, March 31, 2009

Kuuliza si ujinga...!!

Naomba kuuliza, Hili ni tunda gani eti?

Una utamaduni wa kula matunda?


Ni swali la kizushi lakini lina umuhimu sana, tathmini.
Mwili haujengwa kwa matofali.

Yaliyojiri...

Hapa baada ya kupata chai mgonjwa huyu wa akili akipayuka yaliyokitoka katika kinywa chake.

Mgonjwa huyu wa akili nilimkuta akipata chai mgahawani kama pichani inavyoonekana.

Hapa baada ya kumaliza chai akisokota bangi tayari kuipuliza, kabla hajaanza kuisokota alikuwa akipayuka ile mbaya bila kujua ni nani saha anayempayukia toka kinywani mwake.
Huku akisisitiza siogopi mtu nalipuliza hapa hapa nje.
Utajiuliza hizo bangi anazipatia wapi na nani anampatia mimi na wewe sote hatuna majibu.